Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

Ee Moyo mpendelevu wa Yesu, ulio daima na utajiri na ukarimu wa huruma isiyo na mwisho. Na ambaye ulimwambia nabii kuwa sikifurahii kifo cha mtu mwovu bali ageuke na kuishi, uniangalie katika unyonge wangu.

Nakushukuru wewe Kwa moyo wangu wote na Kwa neema za pekee ulizonijalia kupitia fadhila za mtumishi wako mteule, Mtakatifu Rita wa Kashia. Je? Nitakurudishia nini, Ee Bwana, kwa upendo ulionijaloa? Ee Mungu wangu sitaacha daima kukushukuru Wewe ambaye daima umekua mwema kwa wote wanaokudharau.

Nawe mpenzi Mtakatifu Rita, nikulipeje fadhila ulizonijalia? Moyo wangu umejaa furaha isiyo kifani. Nitakushukuru bila mwisho. Ee mtakatifu mwema, uliye


karibu na Bwana wetu; nipelekee Shukrani zangu kwake na kwako na kuwa daima nitaichukia dhambi ili niendelee kufaidi huruma yake na maongozi yake ya mbinguni.

Baba Yetu3, Salamu Maria3 na Akukuzwe Baba3

Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka . Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete ; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Hispani wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako ; Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.

Kiongozi : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Ritha.

Wote: Kwa muhuri wa upendo na mateso.

Tuombe;

Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . Amina

Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)