SIKU YA KUMI NA MBILI (Siku ya tatu ya shukrani)
Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ee Mungu wangu mpendwa, ambaye huwaachi wanye kukutumaini na wenye kukuamini wapate mateso, bali kwa upendo wasikiliza sala zao. Toka kilindini mwa moyo wangu nakutolea shukurani zangu za daima kwa fadhila ulizonijalia kwa maombezi ya mtumishi wako uliyemchagia, Mt Rita. Pokea ,Ee Bwana Yesu, shukurani zangu za dhati, zitokazo kama harufu nzuri ya sadaka. Pokea kupitia mikono ya Mt Rita. Ee Yesu mpenzi, nisaidie ili daima niwe macho kupokea ukarimu wako, wema wako na huruma yako
Pamoja nawe,Ee Mtakatifu mtenda miujiza , ambaye jina lako linatukuzwa kwa furaha kubwa dumiani kote na ambaye maombezi yako huleta miujiza; pokea shukurani zangu toka kilindini mwa moyo wangu. Ningetamani kila mtu akujue; watu wote wakupende. Kwani watu wote wangetambua nguvu zako za mbinguni
Ee nyota angavu ya Shirika la Mt Augustino; katika kutoa shukurani kwa mema niliyopata kwa fadhila nyingi, nitaeneza kwa watu wote ibada yako;nikiwaambia watu kuwa wewe kweli ni Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana, mwombezi wa walio kata tamaa, mwombezi wa wote waliopoteza matumaini ya dunia hii
Baba Yetu3, Salamu Maria3 na Akukuzwe Baba3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete ; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispani wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako ; Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
Kiongozi : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Ritha.
Wote: Kwa muhuri wa upendo na mateso.
Tuombe;
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (Ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments