SHUKRANI KWA HESHIMA YA MAOMBEZI YA MTAKATIFU RITHA WA KASHIA

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

Baba wa milele! Ambaye huruma yako haina mwisho, na wema wako ni wa milele. Niangalie nikikusujudia kwa unyenyekevu mbele ya kiti chacko cha Enzi kitukufu. Nainua kutoka chini ya moyo wangu utenzi wa kukushukuru kwa upendo ulionijalia kupitia mtumishi wako Rita wa Kashia. Natambua eeh Mungu wangu kuwa sistahili kupata fadhila ulizonikirimia na kwa kutokujali mapungufu yangu bali umenisikiliza sala yangu kwa maombezi ya mtakatifu Rita wa Kashia.

Ee mtakatifu Rita mfanya miujiza maarufu wa kanisa katoliki; kwako ninakutolea shukrani zangu za dhati. Kinywa changu hakina maneno ya kutosha ya kueleza jinsi ninavyojisikia moyoni mwangu. Ee mtakatifu mpenzi;ni kweli kwamba wote wanaotumainia maombezi yako hawakatishwi tamaa. Nijaze daima neema ambayo naweza kupata kupitia huruma ya Mungu na unijalie ulinzi wako katika maisha na kifo.

Baba Yetu3, Salamu Maria3 na Akukuzwe Baba3

Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete ; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.


Hispani wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.

Kiongozi : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Ritha.

Wote: Kwa muhuri wa upendo na mateso.

TUOMBE;

Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . Amina

Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)