NOVENA SIKU YA TATU
Kwa jina la Baba,na la Mwana,na la Roho Mtakatifu.Amina
Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa mapumziko,huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu,najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Ritha,unaye ng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za kanisa katoliki,natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini,kwa hamu nangojea,kupata kile nikiombacho (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungi kupitia Mtakatifu Ritha)
Nifikshie ombi langu kwa Yesu wa msalaba.Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopata majaribu,kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa,uliyomtolea Mungu wana wako,ukiomba wasinajisiwe kwa dhambi.Uniombee kwa Mungu.Hicho ni kifo dinicha moyo wako.
Kupitia mateso ambayo Bwana Yesu kristo aliruhusu yakupate ili utakaswe katika majonzi yako,kwa njia ya majiribu mengi yaliyokupata na sadaka nyingi ulizotoa,uniombee ili nijaliwe kupewa ombi langu ninalongojea kwa hamu.
Baba Yetu(3),salamu maria(3)na atukuzwe Baba(3)
Kwa njia ya Mtakatifu Ritha ;homa,madonda na tauni ,viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke umewasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana wafu wanarudishiwa uhai
kwa maombezi yako;radi,tetemeko la ardhina moto havina nguvu.kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana.Watu wengi wanaimba sifa zako.Kashia hutukuza jina lako unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa Mungu Mtakatifu,na kwa mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi : umemtia alama,ee Bwana mtumishi wako Rita
Wote: kwa mhuri wa upendo na mateso
TUOMBE
Ee Mungu uliyekubali kutawadha Mtakatifu Ritja kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.Tunakuomba kupitia maombezi yake neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya metso yako,ili tupate tuzo uliotuhadia kwa wapole na wanaoteseka.Unayeishi na kutawala daima na milele Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments