NOVENA SIKU YA NNE
Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Ee Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana,na wakili wa waliokata tamaa.Hizi ni sifa safi zenye kujaa tumaini kwa roho zenye kujaribiwa na uchungu.Kwako wewe Mtakatifu Rita wa kashia,ambaye wakati tunapojikuta pweke katika maisha yetu,tunapozungukwa na huzuni na kifo,wewe watujia kama mtunza bustani kutoka mbinguni kutuletea ndani ya mioyo yetu iliyokauka tumaini na maji yaliyo hai.
Ee tumaini la moyo wangu ulikauka kutokana na msongo mkubwa wa huzuni;uzito wa maafa umenielemea,mashaka yananiogofya na sijui nielekee wapi kutafuta msaada ninaohitaji.kwako wewe Rita mwema,ninakuamini sana na kukutegemea;nakujia nikiwa na uhakika utanisikiliza. Kwa nguvu ya maombezi yako
mbele ya kiti cha enzi cha Mungu,natumaini kusikilizwa katika ombi langu (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita)
Jionyeshe tena kuwa u mwenye nguvu na huruma.Nithibitishie pia kuwa ni kweli kama wafuasi wako wanavyokukili kuwa Mtakatifu wa yale yaliyoshindikana, na wakili wa waliokata tamaa.
Baba Yetu(3), Salamu Maria(3) na Atukuzwe Baba(3).
Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako;radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu.kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako.Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu,na kwa Mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi : Umemtia alama, Ee Bwana,mtumishi wako
Rita. Wote :kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE:
Ee Mungu,uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso.Tunakuomba kupitia maombezi yake,neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako,ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wananoteseka.Unaeishi na kutawala,daima n milele.Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments