NOVENA SIKU YA PILI
Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina
Ewe mfanya miujiza Mtakatifu Rita wa Kashia. Naona njia ya maisha yako imejaa majaribu na miiba mingi inayochoma, ambayo nahofia imepasua moyo wako vipande vipande. Ee Rita uliye kweli shahidi wa maumivu makali. Uliyeonja tone kwa tone, hadi ukamaliza kikombe chote cha maumivu makali. Nafikiria juu ya moyo wako uliochoka kabisa. Ninakugeukia na kumwomba Mungu kwa maombezi yako (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Wewe unajua maana ya moyo unaovuja damu. Unajua pia kifodini cha roho. Umeumizwa sana na kuteseka sana. Kwa njia ya mateso hayo nakuomba unisaidie katika mahangaiko yangu. Jesi kweli kwamba wakati huu mgumu, Bwana wetu Yesu
ametuandalia njia ya kujipatia neema; kupitia miujiza ambayo binadamu wanaweza kukuomba kwa matumaini na kwa maombezi yako wakafanikiwa?
Ee Mtakatifu mpenzi, iangalie roho iliyopondeka inayolia na kuhuzunika mbele yako. Ninakutumainia, Ee Mtakatifu Rita. Niombee kwa Yesu mbinguni ili nipate kupokea yote ninayomwomba Mungu kwa maombezi yako yenye nguvu.
Baba Baba Yetu (3), Salamu Maria (3), Atukuzwe Baba (3)
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi: Umemtia alama, Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidi kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments