NOVENA SIKU YA KWANZA
Kwa jina la Baba,na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee Mtakatifu Rita mfanya miujiza,uniangalie kwa macho yako yenye huruma,mimi ninaye teseka na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu umezungukwa na miiba. Yaonr macho yangu, ee Mtakatifu Rita,kuwa hayatoki machozi tena kwani machozi mengi yamenitoka!
Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya maisha yangu? Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu wa jina hilo, kwa kunijalia toka kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita).
Kila mtu anasifia utakatifu wako. Kila mtu anasimulia maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa njia yako. Je,mimi tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uniombee kwa Bwana Yesu ili anionee huruma na kunisaidia katika masumbuko na mahangaiko yangu. Kwa maombezi yako, Ee Mtakatifu Rita,niweze kupokea kile ambacho moyo wangu unatamani sana.
Baba yetu ×3 Salamu Maria ×3 na Atukuzwe Baba ×3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita:- homa,madonda na tauni,viini vya maradhi mbalimbali,mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu , viziwi, bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako:- radi,tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego yote,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako . Kashia hutukusa jina lako. Unawasaidia vipofu , viziwi, bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu na kwa Mwanae ziwe sifa,utukufu na heshima,sifa kwa karne zote za pendo la milele. Unawasaidia vipofu , viziwi, bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Kiongozi : Umemtia alama Ee Bwana,mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako,ili tupate tuzo ulilotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala,daima na milele. Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments