NOVENA SIKU YA SABA
Kwa jina LA Baba, nala Mwana, nala Roho Mtakatifu . AMINA.
Ee mpedwa Rita, ambaye maisha yako yalikuwa yahuzuni. Nielekezee uso wako wa huruma mimi mwenye maumivu makali. Naomba sala zangu, uchovu wangu na kuchechemea kwangu viufikie moyo wako mpole ili uweze kufunguliwa kwangu. Huruma yako ambayo wakati wote uliionesha kwa Jiran, maneno ya aman na faraja, na ushauri Mtakatifu uliowapa watu wote vinivute kukuelekea wewe uliye katika mbingu na unakoishi na kuwa mwombezi wa watu wote waliokata tamaa.
Mbele ya miujiza yako mikuu, kifo kinarudi nyuma, vipofu wanapokea nuru, viwete wanasimama, waliopooza wanaponyeshwa na ulemavu wote wa roho na mwili unaondoka kabisa. Je! Nipo peke yangunjsiyefarijiwa na maombezi yako? Sitaamini wala siwezi kuamin hivyo. Nam naamini kwa dhati usimamizi wako na maombezi yako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ninamatumaini makubwa kuwa nitapata amani, moyoni wang, utulivwana fadhila ninazoomba nitajaliwa, [ hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita]
Baba yetu×3, Salam Maria×3, na Atukuzwe Baba×3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita~ homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
Kwa maombezi yako~ radio, tetemeko LA ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete ; watoto wanaomba sana na watu unawarudishia uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo wa mambo yaliyoshindikana, watu wengi wanaimba sifa zako Kashia hutukuza jina lako; Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu, nakwa mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.
Kiongozi: Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa muhuri wa upendo na mateso.
Tuombe:
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohon mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yako, neema za kusamehee adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa Wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . Amina
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments