NOVENA SIKU YA SITA
Kwajina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Nafahamu kwa sababu ya dhambi zangu sala zangu zimefunikwa na wingu zisiweze kufika katika kiti chako cha enzi. Dhambi zangu ni sababuya adhabu zangu kubwa. Sina ujasiri wa kuelekeza sauti yangu kwa YESU. Kwakua mara nyingi sikuthamini huruma yake. Na sasa naiona nguvu yake kuu na ya haki. Mkono wake wa haki umenielekea. Natambua kwamba sistahili baraka za msamaha wake kwani nimegubikwa na huzuni kubwa. Pasipo na matumaini nayalilia madhambi yangu.
Niambie Mtakatifu Ritha, Je, niendelee kukata tamaa? Hapana. Bwana wetu YESU KRISTO amekuteua kuwa mtetezi wake mwenye nguvu ili uniombee kwa Yesu wangu aliye juu,msamaha kwa makosa yangu makubwa na nia safi ya kumtotendea dhambi tena.
Kwa uamuzi huu thabiti,wa midomo yamgu na moyo wangu,nakuelekea wew. Eee Mtakatifu mtenda miujiza,uniombee kwa Bwana Yesu fadhila ambazo nazihitaji sasa ( hapa omba hitaji lako unalotaka kumuomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita) Katika muda huu wa uchovu mkubwa,huzuni na kuachwa pweke, Ee Rita, neno lako kwa Yesu litafungua huruma na msamaha wake. Sema neno na Yesu atakusikia.
Baba Yetu 3, Salamu Maria 3 na Atukuzwe Baba 3.
Kwa njia ya Mtakatifu Rita ~ homa, madonda na tauni,viini vya maradhi mbalimbali mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Kwa maombezi yako : radi tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utukufu wako mitego yote ,hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete : watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jia lako. Unawasaidia vipofu,viziwi,bubu na viwete:watoto wanaomba sanana wafu wanarudishiwa uhai
Kiongozi : Umemtia alama ,Ee Bwana mtumishi wako Rita.
Wote : Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE :
Ee Mungu, uliyekubali kutawadha Rita kwa neema,hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake ,neemaza kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako,ili tupate tuzo uliotuahidia kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)

0 Comments