NOVENA SIKU YA NANE

Kwa jina la Baba,na la Mwana, na la Roho Mt. Amina

Ewe kielelezo kitakatifu cha Msalaba Mtukufu, ninapokuona ukiwa umesujudu mbele ya miguu mitakatifu ya Bwana,ninapotafakari paji la uso wako lililojeruhiwa kwa mwiba uliotoka ktk taji la miiba la Yesu Kristo, mchumbawako mpendwa, imani yangu kwako inachanua kwa namna ya ajabu. Wewe ni mtumishi mteule wa Mungu. Mungu amekuzawadia alama ya ufalme wake akakutakatifuza na kukufanya uwe mali yake kabisa .

Hivyo sikukosea nilivyoweka imani yangu yote kwako,na nilipojiweka kabisa chini ya ulinzi wako wenye huruma nyingi. Na sasa ni wakati mzuri wa kunisaidia, ukiyajua mahitaji na misaada ninayoomba kutoka kwako. Naamini sala hii kwako wewe mama mpenz sana haitapotea bure.

Wew uliye mfanya miujiza, mfadhili wa mambo ya mbinguni, unayetegemewa na wanadamu wote. Ninakuomba na kukusihi kwa mastahili ya pendo lako kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, uniombee ili nijaliwe haya niombayo ( hapa omba hitaji lakounalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Ritha) Mungu hakukatalii wew kitu chochote; kwa maombezi yako,miujiza hufanywa,neema na fadhila maalumu hupatikana. Hivyo, kwa moyo wangu wote na matumaini ya dhati,ninasubiri nikitegemea kupata haya niliyoomba kwa Bwana Mungu.

Baba Yetu 3, Salamu Maria 3 na Akukuzwe Baba 3

Kwa njia ya Mtakatifu Rita; homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa maombezi yako: radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu, kwa utakatifu wako mitego yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete; watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Hispani wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa zako. Kashia hutukuza jina lako ; Unawasaidia vipofu viwete bubu na viziwi, watoto wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.

Kwa Mungu Mtakatifu, na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za Pendo la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete , watoto wanaomba sana na wafu unawarudishia uhai.

Kiongozi : Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Ritha.

Wote: Kwa muhuri wa upendo na mateso.

Tuombe;

Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi yake, neema za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia kuwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele . Amina

Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia……. (ipo mwisho wa sala zote)